Rais wa Marekani Joe Biden anasema alijiondoa katika azma yake ya kugombea tena urais kwa sababu alihofia kwamba vita vya ndani ya chama kuhusu kugombea kwake vingekuwa "usumbufu wa kweli" kwa wademocrat na kwamba kipaumbele chake kikuu kilikuwa kumshinda Donald Trump mnamo Novemba.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu aache kugombea , Biden mwenye umri wamiaka 81, alisema "hana tatizo kubwa" na afya yake. Alilaumu utendakazi wake duni katikamdahalo kwa kuwa mgonjwa wakati huo, na akatupilia mbali wasiwasi kuhusu umri wake na hali yake yakiakili.
Rais wa Marekani aliahidi kumfanyia kampeni Kamala Harris akisema atafanya chochote ambacho makamu wake "anafikiri naweza kufanya kumsaidia pakubwa".
"Lazima, lazima, lazima tumshinde Trump," aliambia shirika la utangazaji la Marekani CBS News.
Bw Biden alisema kama angeendelea na kampeni yake, kinyang'anyiro cha urais kingekuwa "na ushindani wa karibu sana".
"Baadhi ya wenzangu wa chama cha Democratic katika Ikulu na Seneti walidhani kwamba ningewaumiza katika kinyang'anyiro," alisema.
"Na nilikuwa na wasiwasi kama ningesalia kwenye kinyang'anyiro hicho, hiyo ndiyo ingekuwa mada. Ungekuwa ukinihoji kuhusu, Kwa nini Nancy Pelosi alisema, kwa nini alifanya hivyo - na nilifikiri itakuwa ni usumbufusana."
Spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Nancy Pelosi aliripotiwa pakubwa kuongoza vuguvugu la kumtimua Bw Biden - madai ambayo hajakanusha haswa - baada ya kusitisha mjadala wake dhidi ya Trump mnamo 27 Juni.
Wakati wa mahojiano yaliyorekodiwa kabla ya kutangazwa Jumapili, Bw Biden alikosea mara kadhaa lakini kwa ujumla alionekana kuelewekazaidi kuliko wakati wa mjadala wa moja kwa moja wa televisheni. Alisisitiza utendakazi wake duni wa mdahaloulisababishwa na ugonjwa - hapo awali pia alitaja uchovu wa safari yandege na ukosefu wa kupumzika kama sababu.
Shinikizo zilipokuwa zikiendelea kupanda, alitangaza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho tarehe 21 Julai.
Mapambano yaliyotarajiwa yakuchukua nafasi yake ya tiketi ya chama cha Democratic hayakutokea na uungwaji mkono wa chama ulishikana haraka nakumuunga mkono Makamu wa Rais Harris, ambaye hadi sasa amemshinda Bw Biden katika kura za maoni.
Rais amesema alinuia kuwa daraja kwa kizazi kijacho alipowaniakuingia Ikulu mnamo 2020.
"Nilipogombea mara ya kwanza, nilijiona kama rais wa mpito. Siwezi hata kusema nina umri gani. Ni vigumu kwangu kuitoa kinywani mwangu."