KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Julai 29.
Katika taarifa ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tano za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni. Kaunti ambazo zitaathirika ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Nyeri, Murang'a, Kiambu.
Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kilimani, Argwings Kodhek na barabara ya Ngong zitakiosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Ogandi Girls, Ndiru, na Arujo katika kaunti ya Homa Bay yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Maeneo ya Miagayuini, Ngooru, Zaina, Jua Kali na Ihwagi katika kaunti ya Nyeri yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Katika kaunti ya Murang'a, sehemu za maeneo ya Maragua, Ichagaki, Nginda, na Gachocho zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Kariminu Dam, Naivasha Road, na Ituramiro Rd katika kaunti ya Kiambu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.