logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Odinga awasili Elgeyo Marakwet kwa mazishi ya Mzee Chirchir Masit

Atazikwa bila bintiye Irene Masit ambaye yuko uhamishoni kwa hofu ya usalama wake.

image
na Davis Ojiambo

Habari13 August 2024 - 09:46

Muhtasari


  • • Masit alikuwa mmoja wa makamishna wanne wa IEBC waliokataa matokeo ya uchaguzi uliopita na huku wengine wakijiuzulu baadaye alikataa kufanya hivyo.
Kinara wa ODM Raila Odinga akwasili kwa mazishi ya Mzee Chirchir Masit, marehemu ni babake aliyekuwa kamishna wa IEBC Irene Masit /13 Agosti 2024.

Kiongozi wa ODM Raila Odinga amewasili Elgeyo Marakwet kuhudhuria mazishi ya Mzee Chirchir Masit ambaye ni babake aliyekuwa Kamishna wa IEBC Irene Masitt aliye uhamishoni.

Mzee Masit atazikwa leo (Jumanne) huko Chepkorio ambapo ibada ya wafu inaendelea.

Atazikwa bila bintiye ambaye bado yuko nje ya nchi baada ya kutoroka kwa hofu ya usalama wake.

Masit alikuwa mmoja wa makamishna wanne wa IEBC waliokataa matokeo ya uchaguzi uliopita na huku wengine wakijiuzulu baadaye alikataa kufanya hivyo.

Hata hivyo baadaye aliondolewa afisini kufuatia mapendekezo ya jopo lililoundwa kumchunguza.

Raila anahudhuria pamoja na Mbunge wa Kapseret Oscar Sudi na gavana wa eneo hilo Wisley Rotich miongoni mwa viongozi wengine.

Viongozi wengine kadhaa wa kisiasa pia wanatarajiwa kuhudhuria.

IMETAFSIRIWA NA DAVIS OJIAMBO 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved