Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini Kenya, Hakuna watu waliothibitishwa kuwa na Mpox nchini humo.
Katika taarifa yake Jumamosi, Wizara ya Afya ilisema kuwa wasafiri 21,350 walikuwa wamepimwa siku iliyoita, na kufanya jumla ya waliochunguzwa kufikia 302,436 tangu kuanza kwa ufuatiliaji.
Ingawa hakuna watu wanaoshukiwa kuwa na Mpox miongoni mwa wageni, katika kipindi hicho hicho, Wizara iliripoti watu watano wapya wanaoshukiwa Kenya.
"Katika kipindi hichohicho, watu watano wameshukiwa kuwa na Mpox. Kwa jumla, watu 29 wameshukiwa," Wizara ya Afya ilisema. "Kati ya hawa, ishirini na tatu (23) wamepima Mpox, wakati watu sita wanasubiri majibu kutoka Maabara."
Wizara ya Afya imewatahadharisha Wakenya dhidi ya kushiriki picha za washukiwa wa Mpox kwenye mitandao ya kijamii, ili kuzuia kuenea kwa habari potofu na kuheshimu faragha ya wagonjwa.
Kenya ilitangaza mlipuko wa ugonjwa wa Mpox mnamo Julai 31, 2024, baada ya mtu mmoja kuthibitishwa katika Kaunti Ndogo ya Taveta, Kaunti ya Taita Taveta.
Mgonjwa amepona, kulingana na MoH, na kuruhusiwa kutoka hospitalini.
Nako nchini Tanzania, Wizara ya Afya imesema hakuna mgonjwa yeyote aliyethibitika kuwa na maambukizi ya Mpox, lakini imesema inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kuzuia ugonjwa huo kuingia nchini na kuimarisha utayari wa kupambana nao.