logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Watu 6 wafariki katika ajali ya barabarani Eldoret-Nakuru

Polisi na wafanyikazi wa Msalaba Mwekundu wako katika eneo la tukio kusaidia kazi ya uokoaji.

image
na Samuel Maina

Habari20 August 2024 - 05:07

Muhtasari


  • •Basi hilo lililokuwa likielekea Nakuru kutoka Kericho, linasemekana kupoteza breki huku dereva akipiga kona mbaya katika eneo hilo lenye mwinuko.
  • •Polisi na wafanyikazi wa Msalaba Mwekundu wako katika eneo la tukio kusaidia kazi ya uokoaji.
Mabaki ya gari lililohusika katika ajali hiyo Jumanne, Agosti 20,2024.

Takriban watu sita wamefariki katika ajali ya magari mengi katika eneo la Migaa karibu na Salgaa kando ya barabara ya Eldoret-Nakuru.

Basi hilo lililokuwa likielekea Nakuru kutoka Kericho, linasemekana kupoteza breki huku dereva akipiga kona mbaya katika eneo hilo lenye mwinuko.

Basi hilo liligonga vizuizi kwenye eneo hilo na magari mengine mbele yake kabla ya kutua kwenye shimo.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Bonde la Ufa Jasper Ombati alisema timu ilikuwa uwanjani kuratibu kazi ya uokoaji.

Baadhi ya abiria walionusurika kwenye ajali hiyo walisema basi hilo lilikuwa likielekea Mombasa.

Polisi na wafanyikazi wa Msalaba Mwekundu wako katika eneo la tukio kusaidia kazi ya uokoaji.

Ajali hiyo ilitokea mwendo wa saa kumi na moja asubuhi.

Takriban watu 40 wamethibitishwa kujeruhiwa.

"Watu waliojeruhiwa wamepelekwa katika Hospitali za Molo na Coptic kufuatia tukio la trafiki barabarani. Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, pamoja na timu ya kukabiliana na mashirika mbalimbali, bado wako katika eneo la tukio kutoa msaada," ilisema taarifa ya Msalaba Mwekundu wa Kenya.

Ni kawaida kwa ajali mbaya kama hizo kutokea katika eneo hilo kunaweza kusababisha msongamano mkubwa wa magari ikizingatiwa kuwa ni eneo lenye shughuli nyingi.

Hili ni tukio la hivi punde zaidi kuripotiwa tangu wikendi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved