logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Baba adukua hifadhidata kughushi kifo chake ili kuepuka gharama za mtoto

Kipf alikiri kwamba alifanya hivyo ili kuepuka majukumu yake ya malezi ya mtoto ya zaidi ya $100,000.

image
na Samuel Maina

Habari22 August 2024 - 13:06

Muhtasari


  • •Jesse Kipf kutoka Kentucky, nchini Marekani, alihukumiwa kifungo cha miezi 81 kwa ulaghai wa kompyuta na wizi wa utambulisho.
  • •Kipf alikiri kwamba alifanya hivyo ili kuepuka majukumu yake ya malezi ya mtoto ya zaidi ya $100,000.

Mwanamume mmoja amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka sita jela baada ya kudukua hifadhidata ya serikali ili kughushi kifo chake, na kujiondoa kwenye mpango wa kulipia malipo ya gharama za mtoto.

Jesse Kipf kutoka Kentucky, nchini Marekani, alihukumiwa kifungo cha miezi 81 kwa ulaghai wa kompyuta na wizi wa utambulisho.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 39 alikiri kuingia kwenye Mfumo wa Usajili wa Kifo wa Hawaii mnamo Januari mwaka jana na kujiwekea taarifa zinazoonyesha kwamba alifariki dunia.

Kisha Kipf akajaza sehemu ya maombi ya kupata Cheti cha Kifo katika Jimbo la Hawaii, na kujiwekea sahihi kama mthibitishaji wa matibabu akijithibitishia kifo chake kwa kutumia sahihi ya dijiti ya daktari.

Ilimaanisha kuwa alifanikiwa kusajiliwa kama mtu aliyefariki dunia katika hifadhidata nyingi za serikali.

Kipf alikiri kwamba alifanya hivyo ili kuepuka majukumu yake ya malezi ya mtoto ya zaidi ya $100,000.

Mdukuzi huyo pia alipata mifumo mingine ya usajili wa vifo na makampuni katika uvamizi usiohusiana na tukio hilo ambao alitekeleza kwa kutumia nambari za siri zilizoibwa katika maelezo ya madaktari na wafanyakazi.

Aligunduliwa kuwa amejitolea kuwezesha wengine kufikia mifumo hiyo kwa malipo na kuuza hifadhidata zilizoibiwa zenye taarifa za kibinafsi kama Nambari za Usalama wa Jamii kwa wahalifu wengine wa mtandaoni.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved