logo

NOW ON AIR

Listen in Live

'Sina siri ya kipekee ya kuishi miaka mingi' - Mwanamume mzee zaidi duniani azungumza

"Kwa nini nimeishi miaka mingi hivyo, sijui hata kidogo," alisema. "Siwezi kufikiria siri yoyote ya kipekee niliyo nayo.

image
na SAMUEL MAINA

Habari26 August 2024 - 09:44

Muhtasari


  • •Tinniswood alikuwa mwanamume mzee zaidi duniani mnamo mwezi Aprili wakati Juan Vicente Pérez Mora wa miaka 114 alipofariki dunia.
  • •"Kwa nini nimeishi miaka mingi hivyo, sijui hata kidogo," alisema. "Siwezi kufikiria siri yoyote ya kipekee niliyo nayo.

Mwanamume mwenye umri mkubwa zaidi duniani ametangaza kuwa hana "siri ya kipekee" kueleza kuhusu kuishi kwake miaka mingi alipokuwa akisherehekea kutimiza miaka 112.

John Tinniswood, ambaye alizaliwa Liverpool tarehe 26 Agosti 1912, aliiambia Guinness World Records "hakujua kabisa" kwa nini ameishi miaka mingi namna hiyo.

Mwanamume huyo ambaye anaishi katika nyumba ya kutunza wazee huko Southport, alikuwa mwanamume mzee zaidi duniani mnamo mwezi Aprili wakati Juan Vicente Pérez Mora wa miaka 114 alipofariki dunia.

Alisema alikuwa "mchangamfu sana wakati wa ujana wake" na "alitembea kweli kweli", lakini aliamini "hakuwa tofauti" na mtu mwingine yeyote, akiongeza kuwa: "Kuishi miaka mingi au michache, ni kitu ambacho huna uwezo nacho."

Bw Tinniswood, ambaye alizaliwa mwaka ambapo meli ya Titanic ilizama, alisema anatimiza miaka 112 "akiwa na matumaini ya kipekee".

"Kwa nini nimeishi miaka mingi hivyo, sijui hata kidogo," alisema. "Siwezi kufikiria siri yoyote ya kipekee niliyo nayo.

"Nilikuwa na shughuli nyingi kama kijana, nilitembea sana ... Ikiwa hilo lilikuwa na uhusiano wowote na umri mrefu, sijui.

"Lakini kwangu, sio tofauti. Hakuna cha upekee hata kidogo."

Bw Tinniswood alizaliwa miaka 20 baada ya klabu yake ya kandanda anayoipenda zaidi ya Liverpool kuanzishwa.

Alikuwa na miaka miwili wakati Vita vya Kwanza vya Dunia vinaanza na alikuwa ametoka tu kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya 27 Vita vya Pili vya Dunia vilipoanza.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved