Kisa cha 14 cha maambukizi ya Ugonjwa wa Mpox chapatikana kaunti ya Uasin Gishu.Wizara ya Afya imeweza kuthibitisha kisa hicho ambacho kinaongeza visa jumla kuwa 14 kufikia sasa humu nchini tangia kukurupuka kwa gonjwa hili.
Waziri wa Afya Dr. Deborah Barasa katika taarifa aliyoitoa mnamo tarehe 17 Oktoba alisema kisa hicho kilipatikana kaunti ya Uasin Gishu.
Visa hivi vya ugonjwa huu vimeweza kupatikana katika kaunti zifuatazo ndiposa kufikisha jumla ya visa 14:
- Nakuru - 2
- Bungoma - 2
- Taita Taveta - 1
- Busia - 1
- Nairobi - 1
- Mombasa - 1
- Makueni - 1
- Kericho - 1
- Kilifi - 1
- Uasin Gishu - 1
Waziri Barasa alidokeza kuwa kati ya visa hivyo,wagonjwa wanane wameweza kupona na watano wanaendelea kupokea matibabu ya kibinafsi hili kuregesha hali salama.
Alidokeza kuwa vile vile ni kisa kimaoja cha kifo kutokana na ugonjwa huu ambacho kilitokea mnamo 11, Oktoba 2024 kutoka kwa mgonjwa mabye alikuwa na maambukizi na kupona na kisha baadae akafa.
Aidha waziri huyo alisema kuwa wamweka mipango kabambe hili kuhakikisha kwamba wamefanya vipimo kwa viingilio vyote vya Kenya kwa nchi za kigeni.Vile vile alisema kuwa wasafiri takriban 1,362,657 wameweza kufanyiwa vipimo kwa viingilio 26 baada ya kukurupuka kwa ugonjwa huu.
Vinginevyo alisema kuwa mahabara ya kitaifa inazidi NPHL inaendelea na juhudi za kufanya vipimo zaidi akisema vipima 244 zimefanyika huku 14 zikiwa na maambukizi na 3 kufika sasa zinazidi kuchunguzwa.