Mihuri hiyo bandia inadaiwa kutumika katika kuendesha ufisadi
wa takribani shilingi bilioni 1.6 katika madai yanayowausisha maafisa wa kamati
ya utendaji wa kaunti CEC na maafisa wakuu waliokamatwa Alhamisi tarehe 24.
Katika uchunguzi wa EACC, maafisa walipata ofisi inayodaiwa
kutengeneza stakabadhi bandia nyumbani kwa mhandisi Victor Kipkemoi Cheruiyot
aliyetoroka na kuwaacha maafisa hao nyumbani wakati wa msako.
EACC inaamini kuwa mshukiwa huyo amekuwa akitengeneza
stakabadhi bandia alizokuwa akitumia kudai malipo ya miradi isiyokuwepo kwa
ujshirikiano na maafisa katika kaunti ya Bomet.
Nyumbani kwa Victor Kipkemoi, kulipatikana pia hati za
ununuzi na malipo zilizodhibitishwa na maafisa wa kampuni mbali mbali pamoja na
hnati za zabuni zinazosubiri kutiwa sahihi.
Vile vile, stakabadhi za maagizo ya ununuzi, hati za malipo
ambazo hazijatumika pamoja na stakabadhi za mahitaji ya kazi mbali mbali za
ujenzi kwa makampuni zinazoshukiwa kuwa ghushi zilipatikana nyumbani kwa
mshukiwa huyo.
Aidha, EACC inaendelea kufanya uchunguzi wa washukiwa kupata
mali ya umma kwa njia za udanganyifu.