logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Uasin Gishu: Shule yawapa wanafunzi 23 mitihani feki ya KPSEA

Sasa hatima ya wanafunzi hao 23 imesalia kwenye giza.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Habari30 October 2024 - 14:35

Muhtasari


  • Naibu kamishna wa Moiben alithibitisha kisa hicho na kusema kwamba mzazi mmoja ndiye aliyepiga ripoti kituoni baada ya kuona utofuati.
  • “Kuna mzazi mmoja alikuja kuripoti kuwa ameona tofauti kwa shule yake ambapo watoto wanafanya mtihani na anadhani kuna vitu vinafaa kufanyika,’ alisema naibu kamishna.

Wakurugenzi wawili wa shule moja ya kibinafsi wametiwa mbaroni baada ya kudaiwa kuwapa wanafunzi mitihani feki ya KPSEA.

Kwa mujibu wa traarifa, shule hiyo ambayo jina lake tumelibana ilikuwa na watahiniwa 23 wa mtihani wa gredi ya 6, KPSEA ambao umebainika kuwa ulikuwa mtihani bandia, tofauti na mitihani iliyosambazwa katika shule zingine kote nchini.

Sasa hatima ya wanafunzi hao 23 imesalia kwenye giza. Naibu kamishna wa Moiben alithibitisha kisa hicho na

kusema kwamba mzazi mmoja ndiye aliyepiga ripoti kituoni baada ya kuona utofuati. “Kuna mzazi mmoja alikuja kuripoti kuwa ameona tofauti kwa shule yake ambapo watoto wanafanya mtihani na anadhani kuna vitu vinafaa kufanyika,’ alisema naibu kamishna.

Haya yanajiri baada ya serikali kupitia Wizara ya Elimu kufichua kuwa haitawapa vyeti watahiniwa wanaofanya mtihani wa KPSEA. Waziri wa Elimu Belio Kipsang katika mahojiano aliangazia kuwa mitihani ya KPSEA ni tathmini na hivyo watahiniwa hawatapokea vyeti.

"Hii ni tathmini, na katika tathmini, watahiniwa hawapati cheti mwishoni. Wewe, badala yake pata ripoti. Kwa hivyo hata katika tathmini hii mtoto atapata ripoti kuhusu maendeleo yake, na shule itapata ripoti kuhusu maendeleo ya jumla ya shule,” Kipsang alisema kwenye taarifa kwa vyombo vya habari.

Zaidi ya wanafunzi milioni 1.3 katika darasa la 6 walianza Tathmini ya Elimu ya Shule ya Msingi ya Kenya (KPSEA) siku ya Jumatatu kote nchini. Tofauti na mitihani ya kitaifa iliyopita, serikali imepunguza uwepo wa polisi ndani ya madarasa


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved