logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Waziri Ogamba aeleza sababu ya kutoelewana baina ya serikali na UASU

Wahadhiri chini ya muungano wao wa UASU walianza mgomo wa pili Jumanne 29.

image
na Brandon Asiema

Habari30 October 2024 - 11:12

Muhtasari


  • Migosi alikuwa anajibu swali la seneta mteule Gloria Orwoba aliyetaka kufahamu ikiwa upungufu katika mgao wa fedha wizara ya elimu unahusiana na upungufu wa sasa unaosababisha kugoma kwa wahadhiri wa vyuo vikuu.

caption

Waziri wa elimu Julius Migosi amesema kuwa mvurugano baina ya wizara ya elimu na muungano wa wafanyakazi wa vyuo vikuu UASU kuhusiana na fomula ya wahadhiri hao  kurejea kazini ni maelewano ya asilia 7 na 10 makundi hayo mawili yalikubaliana katika mkataba.

Waziri Migosi akiwa mbele ya seneti kujibu maswali ya maseneta kuhusu wizara yake mnamo Jumatano amesema takwimu za fedha ambazo serikali inafahamu ikilinganishwa na fedha zinazohitajika na UASU zinatofautiana na shilingi bilioni 5.

Migosi alikuwa anajibu swali la seneta mteule Gloria Orwoba aliyetaka kufahamu ikiwa upungufu katika mgao wa fedha wizara ya elimu unahusiana na upungufu wa sasa unaosababisha kugoma kwa wahadhiri wa vyuo vikuu.

Waziri Migosi amesema kuwa taifa linakabiliwa na upungufu kwa ujumla katika bajeti ya taifa kwa kila wizara akilaumu kuangushwa kwa mswada wa fedha wa mwaka 2024/2025 kuwa chanzo cha changamoto zinazoshuhudiwa.

Akizungumzia swala la mgomo wa wahadhiri, waziri huyo amesema kuwa wizara itafanya mkutano na UASU Jumatano mchana kujadili namna ya kutatua makubaliano ya ongezeko la asilimia 7 na 10 baada ya kukosa fedha hizo.

Kulingana na Migosi, mkutano wa Jumatano unalenga kuwepo kwa makubaliano baina ya wizara na UASU kukubaliana kiwango kingine cha fedha kitakachowakilisha asilimia saba na kumi kwa kulinganisha na idadiya miaka mkataba huo utadumu.

Mkutano baina ya wizara ya elimu na UASU unajiri siku moja baada ya wahadhari ambao ni wanachama wa UASU kurejelea tena mgomo mwezi mmoja baada ya kuusitisha.

Muungano wa UASU umerejelea mgomo siku ya Jumanne baada ya kulalamikia serikali kukosa kutimiza ahadi ya maelewano ya kurejea kazini ya tarehe 26 Septemba.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved