Mwili wa mwanafunzi wa miaka 19 aliyetoweka tarehe 25 Oktoba wapatikana katika mto Mathioya kaunti ya Murang'a.
Jackline Wangui Gichuru, ambaye ni mwanafunzi wa shule ya upili ya Kamacharia Girls alikuwa amechukuliwa shuleni na bibi yake,baada ya kupata habari kuwa alikuwa ameugua akiwa shuleni ndiposa akapate matibabu ya haraka.
Inaarifiwa kuwa baada ya kufika nyumbani Jackline alielekea moja kwa moja kupumuzika mwendo wa saa mbili.Baada ya nyanya yake kwenda kumuangalia alimkosa na kuanza kumtafuta asijulikane aliko.
Mwili wa msichana huyo ulipatikana ukielea katika mto Mathioya kabla ya kuchukuliwa na kupelekwa kwenye makafani.
Aidha, polisi walianzisha uchunguzi kuhusiana na kifo cha msichana huyo.Hili linajiri siku chache kukiwa na hatari ya usalama kwa wanawake na wasichana na ambapo mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yakimtaka rais kutangaza mauaji haya kama janga la kitaifa.
Taifa kwa mujibu wa pilisi, limeweza kuandikisha visa takriban 97 vya mauaji ya wanawake kwa kipindi cha chini ya miezi mitatu.
Hulka kama hii ya visa vya wanafunzi wa shule za upili kupoteza maisha kwa njia tatanishi zinaendelea kukidhiri wakati huu wanafunzi wamo likizoni kwa niaba ya mtihani wa kitaifa.