logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Safaricom imekanusha madai ya kushirikiana na polisi kufichua maelezo binafsi ya wateja

Ni madai ambayo vile vile idara ya DCI imekanusha vikali wakisema kwamba ikiwa wanataka kupata maelezo ya binafsi ya mtu, huwa wanaelekea mahakamani na kupata agizo.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Habari01 November 2024 - 15:01

Muhtasari


  • Ni madai ambayo vile vile idara ya DCI imekanusha vikali wakisema kwamba ikiwa wanataka kupata maelezo ya binafsi ya mtu, huwa wanaelekea mahakamani na kupata agizo.



Kampuni ya mawasiliano ya Safaricom imejitokeza kimasomaso na kukanusha vikali madai kwamba wanashirikiana na idara za usalama nchini kufichua maelezo ya kibinafsi ya wateja wake.

Kupitia barua kwenye kurasa zake mitandaoni, Safaricom ikikanusha taarifa hizo ikisema kwamba inazingatia kwa njia ifaayo usalama wa maelezo ya kibinafsi ya wateja wake wote.

“Safaricom inafahamu mijadala inayoendelea kuhusu uvumi kwamba inashirikiana na idara za kiusalama kufichua maelezo ya faragha ya wateja wetu na tungependa kusema yafuatayo, kwamba tunaheshimu sana wateja wetu na tunafuata kikamilifu sheria za nchi kuhusu usalama wa data za watu. Kutokana na hilo, hatuwezi kufichua maelezo ya kibinafsi ya mteja isipokuwa pale tutakapotakiwa kufanya hivyo kupitia barua ya mahakama,’ walisema.

Taarifa hiyo inafuatia ufichuzi wa gazeti la Daily Nation lililodai kuwa polisi wamekuwa wakitumia data za simu za mkononi kuwasaka na kuwakamata washukiwa kwa usaidizi wa mawasiliano ya simu, hasa wakati wa maandamano ya Gen Z ambapo zaidi ya waandamanaji 60 waliuawa.

Kulingana na makala iliyochapishwa Jumanne, Safaricom ilipachika Neural Technologies, mfumo wa usimamizi wa data katika mifumo yake ya ndani inayoruhusu huduma za usalama bila vikwazo kwa ufikiaji wa data za simu za Wakenya katika wakati halisi, madai ambayo telco ilikanusha.

Ni madai ambayo vile vile idara ya DCI imekanusha vikali wakisema kwamba ikiwa wanataka kupata maelezo ya binafsi ya mtu, huwa wanaelekea mahakamani na kupata agizo.

“Suala la polisi kula njama na watoa huduma za simu hatufanyi hivyo kabisa, tukipenda kupata taarifa kutoka kwa watoa huduma tunafanya hivyo kwa njia halali, tunaenda mahakamani tunaapa na kuhudumia. agizo hilo kwa watoa huduma ni baada tu ya kupata maagizo ndipo tunapopata watoa huduma wafanye kazi nasi."

"Tunapoendelea na uchunguzi wetu, hatutegemei kabisa simu za rununu inachangia asilimia moja ya uchunguzi wetu na katika hali nyingi ambapo tunaweza kufanya uchunguzi kwa ufanisi, ni matokeo ya uchambuzi wetu wa kitaalamu na ukusanyaji wa ushahidi wa DCI na NPS hawategemei kabisa watoa huduma za simu," Mkurugenzi huyo alisema wa Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mohamed Ibrahim Amin.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved