DHEEBU la PEFA limeonekana kuenda kinyume na
madhehebu mengine mengi humu nchini kuhusiana na suala la kupokea na kurejesha
sadaka na matroleo yote yanayoletwa na wanasiasa.
Katika mkutano na waandishi wa Habari, mchungaji wa
PEFA alisisitiza kwamba kanisa hilo haliwezi kukataa kupokea sadaka kutoka kwa
wanasiasa kwa sababu hawawezi kujua sadaka hizo kama ni mafao ya ufisadi au la.
Msimamo wao unajiri wiki moja tu baada ya muungano wa
makanisa nchini NCCK kupitisha kwa kauli moja kutokubali sadaka kutoka kwa
wanasiasa na pia kurejesha zile ambazo zimeshapokelewa.
Kanisa hilo limesema kuwa litaendelea kufanya kazi na
tabaka la kisiasa, kuwakaribisha wanasiasa katika matawi yake 3,000 kote
nchini.
“Kuna
madhehebu ambao wamesema kwamba sadaka watakuwa wanaangalia, kunai le watakuwa
wanakubali, kuna ile watakataa lakini sisi kama ushirika wa PEFA bado hatuna
mbinu ya kukagua ni gani inakubalika na ni gani inakataliwa. Kwa hivyo kuanzia
sasa hivi kuendelea mbele bado tutazipokea sadaka zote na tutaziweka katika
kazi,” mchungaji aliambia waandishi wa habari.
“Sisi
kama PEFA haturudishi sadaka, kwa sababu hatuwezi kujua hizi sadaka zimetoka
wapi unless tuwe na mikakati ya kuziangalia. Tunashukuru wote ila tunasema
sadaka ikitolewa isitangazwe,” aliongeza.
Hii ni licha ya upinzani wa umma ambao makanisa ya
Kikristo yamepokea kuhusu hili. Wakenya wengi wamedai kuwa michango hiyo
inaibua masuala ya kimaadili ambayo yanaweza kuchafua taswira ya Kanisa nchini
Kenya.
Msimamo wao unakuja huku makanisa ya Kikatoliki na
Kianglikana yakitoa maagizo kwa makanisa yao kusitisha kuchukua michango ya
pesa kutoka kwa wanasiasa na kuelekeza matawi mahususi kurejesha michango ya
kisiasa.
Mjadala kuhusu michango ya kisiasa makanisani ulianza
Novemba 19, wakati Kanisa Katoliki lilipoelekeza makasisi katika Kanisa
Katoliki la Soweto kurejesha Ksh5.8 milioni kutoka kwa Rais William Ruto.
Rais Ruto alitoa Ksh 600,000 kwa Kanisa Katoliki la
Soweto jijini Nairobi kwa wanakwaya na Ksh2 milioni ambazo zingetumika kujenga
nyumba ya baba.
Pia aliahidi kuchangia Ksh3 milioni za ziada ambazo
zitatumwa kwa akaunti ya kanisa kununua basi la kanisa. Wakati wa hafla hiyo,
Gavana Sakaja alitoa Ksh200,000 kwa kanisa moja