Mbwa, panya na nyuki wamegundulika kuwa wanyama wa
pekee wenye uwezo wa kugundua magonjwa ya vwanadamu.
Mbwa
Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa na BBC, mbwa ana uwezo wa kugundua magonjwa ya wanadamu kwa kutumia mnuso, kulamba na hata kujaribu kutafuna madoa kwenye ngozi ya wamiliki wao, ambayo baadaye hugunduliwa kuwa ni saratani ya ngozi.
Mbwa pia anaweza kutambua magonjwa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ugonjwa wa kutetemeka kutokana na shida ya ubongo, saratani ya kibofu cha mkojo na malaria.
Kifafa na kiwango cha chini cha sukari katika damu kwa wagonjwa wa kisukari vinaweza pia kufichuliwa na mbwa maalumu waliofunzwa.
Inaaminika uwezo wa mbwa wa kunusa harufu, ni mara
10,000 zaidi ya uwezo wa binaadamu.
Wanaweza hata kutumia pua zao kuchunguza harufu mpya.
Panya
Panya wana uwezo mzuri
katika kugundua harufu fulani.
Wapo panya wamepewa
mafunzo ya kutambua harufu ya vilipuzi vya ardhini nchini Msumbiji.
Pia wamethibitika kuwa na uwezo mzuri katika uchunguzi wa
kimatibabu, hugundua kifua kikuu katika sampuli za makohozi ya watu wanaohisiwa
kuwa na ugonjwa huo.
Panya ni wepesi na huchukua dakika 20 tu kukagua sampuli 100 za
wagonjwa.
Wanatumia hisia zao za
kunusa kugundua dalili za kemikali ya kifua kikuu katika sampuli.
Hilo huwafanya panya hao waliofunzwa kuwa chaguo muhimu pale
muda, vifaa na pesa vinapokuwa haba katika hospitali au maabara.
Panya wanatambua kwa
usahihi visa vya TB kwa 81%.
Nyuki
Nyuki wanaweza
kugundua dalili za magonjwa fulani kupitia sampuli, ikiwa ni pamoja na saratani
ya mapafu, kifua kikuu na covid-19.
Wana uwezo mkubwa wa kunusa harufu ndogo sana, na hilo huwafanya
kuwa na uwezo wa kugundua mabadiliko ya kemikali kama vile mbwa na panya.
Uwezo huu huwafanya nyuki kuwa muhimu kugundua magonjwa kwa njia
sawa na wanyama wengine.
Ukubwa wao unaweza kuwafanya kuwa chaguo bora
na la gharama nafuu kwa "uchambuzi" wa haraka wa sampuli.
Wana uwezo wa kugundua mabadiliko madogo katika mfumo wa harufu kupitia kemikali za mtu.
Wanaweza kutambua
mabadiliko madogo katika kemikali ambayo mwili hutoa kwa viwango vya chini
sana, hata wakati mtu akiwa na afya.
Pumzi ya mwanadamu inatoka takribani kemikali za gesi 3,500.
Muundo na mkusanyiko
wa kemikali ambazo mwili hutoa hubadilika kulingana na afya ya mtu na kemikali
hizo hubadilika ikiwa mwili unapigana na maambukizi au kukabiliana na tatizo la
kiafya.