logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Kisumu Intern!" Larry Madowo akejeli Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu

Madowo mnamo Jumapili jioni alikejeli maandishi ya kutambulisha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu.

image
na Samuel Mainajournalist

Habari16 December 2024 - 09:39

Muhtasari


  • Mwangaza uliomulika maandishi hayo iliwaka hadi “KISUMU INTERN” huku maandishi mengine “..ATIONAL AIRPORT” yakiwa hayawezi kuonekana vizuri.
  • Katika miaka ya hivi majuzi, mwanahabari Larry Madowo amekuwa na sauti kubwa kukosoa hali ya viwanja vya ndege vya Kenya.


Mwanahabari maarufu wa kimataifa kutoka Kenya Larry Madowo mnamo Jumapili jioni alikejeli maandishi ya kutambulisha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu.

Mwanahabari huyo wa CNN alikuwa akisafiri kwa kutumia uwanja huo wa ndege baada ya kushinda siku nzima mjini Kisumu alipotambua jinsi maandishi hayo yalivyomulikwa kwa sehemu tu.

Mwangaza uliomulika maandishi hayo iliwaka hadi “KISUMU INTERN” huku maandishi mengine “..ATIONAL AIRPORT” yakiwa hayawezi kuonekana vizuri kwa vile hayakuwa na mwanga.

Larry alichukua picha ya maandishi hayo na kuyafanyia mzaha akisema, "Usiku mwema kutoka Kisumu Intern."

Aliendelea kutania kuwa huenda uwanja huo wa ndege ulikuwa kwenye hali ya kuhifadhi nishati.

"Je, iko kwenye hali ya kuokoa nishati?" Alisema.

Tazama maoni ya baadhi ya Wakenya kwenye Facebook;

Anne Nyambura: Same thing at Moi International Airport, Mombasa.

Kimutai.co.ke: Hiyo ni decoration, it lights on turns at an interval of 1 hour, you could hang around kidogo and the remaining letters could light up.

Solomon Muingi: Hii pia Adani aje kufix hiyo taa?

John Marenya: Our Kisumu intern is in training to be an international airport in future.

Felix Oluoch Okoth: The rest of the letters are silent.

Katika miaka ya hivi majuzi, mwanahabari Larry Madowo amekuwa na sauti kubwa kukosoa hali ya viwanja vya ndege vya Kenya, haswa Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA).

Mwaka huu na mwaka jana alilalamikia sana kuhusu kukatika kwa umeme na paa kuvuja kwenye uwanja huo wa ndege wa kimataifa, akitaka serikali kuboresha viwango


 



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved