Wanaume wawili wamepoteza aushi yao kufuatia ajali ya kuangukiwa na ukuta waliokuwa wakipata rangi eneo la Runda, jijini Nairobi.
Katika kisa hicho, kwa mujibu wa taarifa ya polisi watu wengine wawili walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya.
Taarifa ya mashahidi na polisi walioshuihudia tkuio hilo ilisema kwamba wanaume hao walikuwa wamekodiwa naraia mmoja kupaka rangi na kupamba ukuta wa eneo la makazi yake.
Walipokuwa wakiendelea na kazi hiyo, mvua ilianza kunyesha na kuwalazimu fundi hao kutafuta hifadhi ya kujikinga mvua kwenye kibanda cha jirani. Katika hali ya mvua kunyesha, ndipo ulipoporomoka na mafundi hao kubanwa na mabati ya kibanda walimokuwa wamejikinga mvua.
Hatimaye, mafundi hao waliokolewa na kukimbizwa katika hospitali ya Kiambu, ambapo wawili walitangazwa kufariki walipofika, polisi walisema. Polisi baadaye walitembelea eneo la tukio kama sehemu ya uchunguzi wa mkasa wa Desemba 17.
Uchunguzi kuhusiana na tukio hilo la Disemba 17 linaendelea kuchunguzwa kwa muhjibu wa mkuu wa polisi katika kaunti ya Nairobi. Ucunguzi huo unaendeshwa na maafisa wa upelelezi kutoka kituo cha polisi cha Gigiri.
Mkuu huyo wa polisi alisema baadhi ya taarifa zimerekodiwa na miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Kiambu ikisubiri uchunguzi wa maiti.
Uchunguzi ungali unafanywa kubaini ikiwa ua uliokuwa
uanapakwa rangi ulikuwa umejengwa kwa kuzingatia ubora unaohitajika.