logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mwanamume abubujikwa na machozi baada ya kuokoa mbwa kutoka kwa moto nchini Marekani

Mbwa huyo hatimaye alipokea matibabu ya majeraha ya moto na hewa ya kaboni dioksidi katika kituo cha uokoaji

image
na Brandon Asiema

Habari10 January 2025 - 13:26

Muhtasari


  • Miller alisema kwamba aligundua uwepo wa mbwa aliyekuwa na majeraha katika upande wa pili wa barabara akiwa chini ya vifusi na mawe.
  • Alimchukua mbwa aliyemwokoa na kumpeleka katika kituo cha uokoaji cha Pasadona akitumai mbwa huyo atakuwa na siku zijazo angavu.


Jamaa mmoja nchini Marekani alishindwa kujizuia kutokwa na machozi wakati alimnusuru mbwa mmoja katika eneo la Altadena ndani ya jimbo la Calirfonia kutokana na kusambaa kwa moto wa nyika manmo Alhamisi, Januari 9, 2025.

Akizungumza baada ya kuokoa mbwa huyo, jamaa huyo kwa jina Rick Miller alisema kuwa alikuwa katika harakati ya kumjulia hali rafiki wake ambaye nyumba yake ilikuwa imechomeka katika moto huyo.

Katika harakati yake hiyo, Miller alisema kwamba aligundua uwepo wa mbwa aliyekuwa na majeraha katika upande wa pili wa barabara akiwa chini ya vifusi na mawe. Miller aliamua kumsaidia mbwa huyo.

“Ni kuhusu kujaliana. Kama kila mtu anahitaji msaada na hivyo….” Miller hakumaliza maneno hayo alipoanza kububujikwa na machozi huku akiomba radhi. ”samahani kwa kulia lakini ni tukio la kihisia.” Alisema Miller katika video iliyorekodiwa na shirika la habari la kimataifa la CNN.

Rick Miller amesema kwamba moto huo wa nyika uliofika hadi kwenye makao ya watu imedhuru ila mtu. Kwa upande wake, msaada anaoweza kutoa ni kkujaribu kuwasaidia watu wengine na viumbe.

“Kama marafiki zangu kupoteza nyumba zao na kupoteza wanyama wao kwa hivyo sisi tunajaribu kusaidiana.”  Aliendelea kusema Rick Miller.

Akiwa na machozi yakimlenga lenga machoni Rick Miller alisema kuwa imeonekana ni kama marafiki wote na familia imepoteza nyumba zao kwa hivyo anawasaidia kwa namna anavyoweza.

Hata hivyo nyumba yao ilinusurika kwa kuwa haikupatwa na moto huo ijapokuwa nyumbani ya rafiki zake mkabala na yao iliteketea.

Rick Miller alimchukua mbwa aliyemwokoa na kumpeleka katika kituo cha uokoaji cha Pasadona akitumai mbwa huyo atakuwa na siku zijazo angavu.

Kituo cha Pasadone kilithibitisha kumpokea mbwa huyo ambaye hatimaye alipokea matibabu ya majeraha ya moto na hewa ya kaboni dioksidi.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved