MBUNGE wa Kikuyu ambaye pia ni kiongozi wa wengi katika bunge la kitaifa, Kimani Ichung’wah amesisitiza kwamba hakuna kauli cyoyote ya kumdunisha itamfanya kukoma kuendelea kumtetea rais William Ruto na serikali ya Kenya Kwanza.
Akizungumza katika bonde
la ufa alipoandamana na rais katika ziara yake ya siku 3 ya kimaendeleo, mbunge
huyo alisema kwamba baadhi ya watu wanatumiwa na wanasiasa kugawanya wananchi
na kuzua chuki dhidi ya rais.
Ichung’wah alisema
kwamba amesikia kwenye mitandao wanamuita ‘bibi ya rais’ lakini akasema hilo
halitamfanya kuacha kutetea serikali ya Ruto na yeyote anamshambulia rais
atapatana na yeye.
“Na mtu wa kucheza na
rais Ruto, tunaangaliana macho kwa macho. Hata waseme eti mimi ni bibi ya rais,
si nasikia huko kwa mitandao wananiita eti mimi ni bibi wa Ruto…si wanajua bibi
wa mheshimiwa rais? Lakini hata wanitukane, mimi ukicheza na hii serikali, na
huyu rais na naibu wake ni mimi na wewe mundu khu mundu,”
Ichung’wah alisisitiza.
Aidha, mbunge huyo wa
Kikuyu alirudha dongo kwa gavana wa Trans Nzoia George Natembeya baada ya
kutishia kumchukulia hatua za kisheria kwa kauli aliyotoa dhidi yake wiki
chache zilizopita katika hafla ya mazishi ya mamake spika wa bunge la kitaifa,
Moses Wetang’ula.
Ichung’wah alitoa tetesi
zenye ukakasi mkubwa kwamba Natembeya alihusika katika utekaji nyara wa watu kipindi akiwa kama RC wa mkoa
wa bonde la ufa.
“Huyo wa kutembea
akikuja nitembee na yeye? Atembee asitembee? Na mmuambie mimi si mtu wa
kutishwa,” Ichung’wah alisema.