IDARA ya DCI imevunja kimya baada ya maafisa wake kushambuliwa na umma katika kaunti ya Kirinyaga walipoenda kumtia mbaroni mshukiwa mmoja.
Kupitia picha na video zilizoenezwa mitandaoni,
maafisa hao waliokuwa ndani ya gari dogo walifumaniwa na umma uliokuwau mejaa
ghadhabu wakitishia kuliteketeza gari lao.
DCI kupitia ukurasa wao wa Facebook walitoa taarifa
kuhusu tukio hilo wakionya umma vikali na kusema kwamba kujaribu kuzuia
makachero dhidi ya kutekeleza majukumu yao ni kosa kubwa kisheria.
Walisema kwamba maafisa wake walimusurika
kushambuliwa na umma, shukrani kwa maafisa kutoka kituo cha polisi kilichopo
karibu na eneo la tukio, chifu na wazee wa nyumba kumi.
“Maafisa
hao walikuwa wametumwa na Afisa wa Upelelezi wa Jinai wa Kaunti Ndogo kumsaka
mshukiwa aliyetoroka.”
“Kundi
la watu wenye ghasia, hata hivyo, walikusanya vikosi na kuwashambulia maafisa
waliokuwa kwenye gari la serikali nambari ya usajili KBZ 684Y, wakitishia
kuiteketeza iwapo hawatamwachilia mshukiwa.”
“Shukrani
kwa polisi wa eneo hilo, chifu wa eneo hilo na wazee wa Nyumba Kumi, ambao
walishinda hali ya wasiwasi na kuwezesha kuwekwa kizuizini kwa mshukiwa,’
DCI walisema.
“DCI
inatahadharisha umma kwamba kuwazuia maafisa wa polisi katika kutekeleza
majukumu yao ya kikatiba ni kosa kubwa la jinai, na mbaya zaidi ni jaribio
lolote la kusaidia kutoroka kwa mhalifu au mfungwa,”
waliongeza.
Kisa hicho kinajiri wakati ambapo serikali imekuwa
ikilaumiwa dhidi ya msururu wa utekaji nyara ambao umekuwa ukifanyika nchini.