KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatatu, Januari 20.
Katika taarifa ya Jumapili jioni, kampuni hiyo ilisema kukatizwa kwa umeme kutatokana na ukarabati ambao utakuwa ukifanyika kwenye mitambo.
Walisema baadhi ya maeneo ya kaunti tatu za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika ni Nandi, Uasin Gishu, na Nyeri.
Katika kaunti ya Nandi, maeneo ya Lessos, Sojoi, na Koisagat yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Kitingia, Kondoo Chereber, Burnt Forest, na Ainabkoi katika kaunti ya Uasin Gishu zitakosa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya Kangocho na Mwanda katika kaunti ya Nyeri pia zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.