
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 22 alikasirishwa baada ya kutopata majibu sahihi mahali ambako begi yake ilikuwa wakati alikuwa anaihitaji.
Mvulana huyo aliyetekeleza kisa hicho cha kushangaza kwa sasa amekimbilia mafichoni. Wazazi wake wawili wamezungumza na wanahabari na kueleza kilichojiri.
Wazazi hao ambao ni wakaazi wa vihiga sasa wanaililia serikali na wahisani kuwasaidi kupata mahali pa kulala na mavazi kwani kila kitu walichomiliki kimeungua ndani ya nyumba.
"Nimepatwa na msibaa huu wa nyumba kuchomwa, na mimi ninaomba wahisani wansaidie maana sina mahali pa kulala. Sababu kila kitu kimeungua, siku ya leo tena naenda kulala kwa baridi. Baridi inanimaliza. Hata tu kitu chochote cha kujifunika hakuna," alizungumza baba mzazi.
"Nyumba imechomwa sababu mtoto alikuwa anataka bagi. Sa zile alikuwa anataka wakati huo, kuchelewa tu kidogo nikapata nyumba imechomwa. Mpaka nilishindwa ni kitu gani kiliingilia ndani. Huyo mtoto ni wa miaka 22, sasa hivi amepotea simuoni," mzazi huyo wa kiume aliendela kuleza masaibu yake.
Mzazi wake wa kike ambaye pia alikuwepo aliitaka serikali kuingilia kati na kumsaidia kupata mahali pa kuishi. Alisisitiza kwamba hana hata mavazi kwani hakuna kilichosazwa kwenye mkasa huo wa moto.
"Sasa mtoto alianza kisirani akachoma nyumba, na mimi sikujua kiini chenye kilifanya akachoma nyumba. Hata mimi nimehuzunika sana nilipopata nyumba imechomeka na kila kitu kimechomeka. Nguo zote zimechomeka sina ata nguo ya kuvaa. ningependa serikali inisaidie kama inaweza nitengenezea mahali penye naishi hata pawe pahali padogo nitashukuru." alieleza mama huyo.