logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Bashasha huku mwanamke akijifungua salama ndani ya treni ya SGR (picha)

KRC ilithibitisha kwamba mwanamke huyo na mtoto wake mchanga wako sawa na salama baada ya tukio hilo la kipekee.

image
na SAMUEL MAINA

Habari22 June 2023 - 03:57

Muhtasari


  • •KRC ilifichua kwamba mwanamke huyo  alijifungua salama kwa usaidizi wa Daktari Indanyenyi Luseso na mhudumu Mary Nyiha ambao pia walikuwa ndani ya treni hiyo.
  • •KRC ilithibitisha kwamba mwanamke huyo na mtoto wake mchanga wako sawa na salama baada ya tukio hilo la kipekee.
alijifungua ndani ya treni ya SGR Jumatano, Juni 21 2023.

Siku ya Jumatano, Juni 21, mwanamke mmoja alijifungua kwa mafanikio akiwa ndani ya treni ya Madaraka Express inayojulikana kama treni ya SGR.

Katika taarifa ya Jumatano jioni, Shirika la Reli la Kenya lilifichua kwamba mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa alijifungua salama kwa usaidizi wa mhudumu wa afya, Daktari Indanyenyi Luseso na mhudumu wa abiria, Bi Mary Nyiha ambao pia walikuwa ndani ya treni hiyo.

Treni hiyo ilikuwa ikielekea mji wa pwani wa Mombasa kutoka Nairobi.

"Tunayo furaha kushiriki hadithi ya kufurahisha ya mama ambaye alikaribisha mtoto kwenye treni ya Madaraka Express ya kusafirisha Abiria hadi Mombasa," taarifa ya KRC ilisoma.

"Tulibarikiwa kuwa na Dkt. Indanyenyi Luseso ambaye alitoa huduma hiyo, akisaidiwa na mhudumu wetu wa Abiria, Bi. Mary Nyiha. Baadaye, alikimbizwa katika hospitali ya kaunti ndogo ya Mariakani kwa usaidizi zaidi wa matibabu," iliendelea.

KRC ilithibitisha kwamba mwanamke huyo na mtoto wake mchanga wako sawa na salama baada ya tukio hilo la kipekee.

"Mama na mtoto wote wako sawa. Tunamtakia heri,"

Shirika la reli pia lilishiriki picha za mama huyo mpya, daktari na mhudumu wa abiria akiwa wamemshika mtoto huyo mchanga huku tabasamu kubwa zikiwa zimeandikwa kwenye nyuso zao.

Abiria wengine wenye furaha tele waliokuwa kwenye kibanda kimoja na mama huyo walionekana wakitazama kwa udadisi wakiwa mbali.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved