Tanzia: Mwenyekiti wa Sameer Group, bilionea Naushad Merali aaga dunia

Naushad ambaye ametajwa miongoni mwa Wakenya tajiri zaidi nchini Kenya atazikwa leo, Julai 3

Muhtasari

Familia ya bilionea huyo imethibitisha kuwa marehemu aliaga Jumamosi asubuhi akiwa nyumbani kwake jijini Nairobi.

Naushad Merali
Naushad Merali
Image: Hisani

Mwanabiashara mashuhuri , Naushad Noorali Merali ameaga dunia.

Familia ya bilionea huyo imethibitisha kuwa marehemu aliaga asubuhi ya Jumamosi  akiwa jijini Nairobi.

Naushad ambaye ametajwa miongoni mwa Wakenya tajiri zaidi atazikwa hivi leo, Julai 3. Amefariki akiwa na umri wa miaka 70

Kupitia ujumbe uliandikwa na shirika la Shia Ithna Ashri Jamaat, jamaa wa karibu na wale wanaosaidia kwa shughuli ya mazishi pekee ndio watahudhuria ibada hiyo.

"Ni ombi la familia kuwa mikakati ya kudhibiti COVID19 izingatiwe  kwa hivyo familia ya karibu na wale wanaosaidia kwenye mazishi pekee ndio watahudhuria. Familia inawashukuru kwa kutii ombi" ujumbe huo ulisema.

Ibada ya jamii na marafiki kumkumbuka Naushad itatangazwa baadae.

Mwaka wa 2015, Forbes ilimuorodhesha marehemu kama nambari 48 kwenye orodha ya Waafrika tajiri zaidi. Alitajwa kuwa na utajiri wa bilioni 39.96 kwa wakati huo.

Marehemu alikuwa mwanzilishi wa huduma ya simu ya Kencell(Airtel kwa sasa)