Koplo Caroline Kangogo ajitoa uhai kwa kujipiga risasi kichwani

Polisi wamekuwa wakimuwinda Kangogo baada yake kutekeleza mauaji ya kinyama dhidi ya wanaume wawili maeneo ya Nakuru na Juja.

Muhtasari

•Inadaiwa kuwa Kangogo amejiuwa kwa kujipiga risasi kichwani akiwa nyumbani kwa wazazi wake maeneo ya Elgeyo Marakwet.

Image: HISANI

Mshukiwa katika mauaji ya watu wawili,  koplo Caroline Kangogo amejitia kitanzi.

Inadaiwa kuwa Kangogo amejiuwa kwa kujipiga risasi akiwa nyumbani kwa wazazi wake maeneo ya Elgeyo Marakwet.

Akithibitisha tukio hilo, kamanda wa polisi maeneo ya Keiyo, Tom Makori amesema kuwa Kangogo alijipiga risasi  kwa kutumia bastola akiwa ndani ya bafu.

Inadaiwa kuwa huenda Kangogo alifika kwao jioni ya siku ya Alhamisi.

Polisi wamekuwa wakimuwinda Kangogo baada yake kutekeleza mauaji ya kinyama dhidi ya wanaume wawili maeneo ya Nakuru na Juja.

Hapo awali, wazazi wa Kangogo walikuwa wamemuomba mwanadada huyo kujisalimisha.

Maafisa wa kukabiliana na uhalifu wametumwa katika eneo hilo.

Hata hivyo, utata umeibuka kuhusu kifo hicho huku baadhi ya watu wakidai kuwa huenda Kangogo hakujitoa uhai mwenyewe.

 

Mengi yatafuata.