Washukiwa wa kigaidi waliotoroka Kamiti wakamatwa Kitui

Watatu hao walikuwa wanaelekea katika nchi jirani ya Somalia

Muhtasari

•Watatu hao,Musharraf Abdalla, Joseph Juma na Mohammed Abdi walikamatwa alasiri ya Alhamisi katika eneo la Mwingi, kaunti ya Kitui.

Musharraf Abdalla, Joseph Juma na Mohammed Abdi wakamatwa wakielekea Somalia
Musharraf Abdalla, Joseph Juma na Mohammed Abdi wakamatwa wakielekea Somalia
Image: HISANI

Wafungwa watatu wa kigaidi ambao walitoroka katika gereza ya Kamiti siku nne zilizopita hatimaye wameweza kutiwa mbaroni.

Watatu hao, Musharraf Abdalla, Joseph Juma na Mohammed Abdi walikamatwa alasiri ya Alhamisi katika eneo la Mwingi, kaunti ya Kitui.

Washukiwa hao ambao walidaiwa kuwa hatari walikuwa safarini kuelekea Garissa walipotiwa mbaroni.

Polisi wamesema watatu hao walikuwa wanaelekea katika nchi jirani ya Somalia.

Abdalla, Juma na Mohammed walitoroka katika gereza hiyo yenye ulinzi mkubwa mnamo Novemba 15 ambako walikuwa wanazuiliwa baada ya kuhusishwa na ugaidi.

DCI ilitoa ahadi ya shilingi milioni 60 kwa yeyote ambaye angetoa habari ambazo zingesaidia kukamatwa kwa washukiwa hao.

Bado haijathibitishwa iwapo kuna yeyote atakayepokea kitita hicho cha pesa kuona sasa washukiwa wameweza kukamatwa.

Haya yanajiri huku walinzi kumi na watatu wa gereza wakiwa wamekatwa kuhusiana na matukio ya wafungwa kutoroka gerezani.

Serikali pia imefanya mabadiliko makubwa katika kitengo cha magereza , ikiwemo kufutwa kazi kwa  mkuu wa magereza Wycliffe Ogalo.

Mengi yanafuata...