logo

NOW ON AIR

Listen in Live

DJ Evolve aondoa kesi ya jaribio la mauaji dhidi ya mbunge Babu Owino

Hii ni baada ya mahakama kuruhusu kuondolewa kwa kesi hiyo na DJ Evolve.

image
na Radio Jambo

Makala14 December 2021 - 13:30

Muhtasari


  • Hii ni baada ya mahakama kuruhusu kuondolewa kwa kesi hiyo na DJ Evolve
  • Hata hivyo atashtakiwa katika shtaka la pili la kujiendesha kwa fujo huku akiwa amebeba bunduki
Babu Owino

Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameondolewa mashtaka katika kesi ambayo alishtakiwa kwa jaribio la kumuua Felix Orinda, almaarufu DJ Evolve.

Hii ni baada ya mahakama kuruhusu kuondolewa kwa kesi hiyo na DJ Evolve.

Hata hivyo atashtakiwa katika shtaka la pili la kujiendesha kwa fujo huku akiwa amebeba bunduki.

Babu alikuwa amejaribu kusuluhisha kesi yake na DJ Evolve nje ya mahakama.

Mbunge huyo alishtakiwa kwa kujaribu kumuua Evolve ambaye alimpiga risasi katika kilabu cha Kilimani, Nairobi, 2018.

Wakili wa familia ya DJ Evolve aliambia mahakama kuwa wako katika hatua za mwisho za mazungumzo.

Hakimu mkuu mkuu Bernard Ochoi alisikia kuwa kitu pekee kilichowazuia ni hati ambazo walipaswa kuwasilisha kwa upande wa mashtaka.

Upande wa mashtaka ulithibitisha kuwa mazungumzo yamekuwa yakiendelea kati ya pande hizo mbili.

Mahakama ilisikia kwamba upande wa mashtaka ulifanya mikutano miwili kati ya Babu na Evolve pamoja na mawakili.

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved