logo

NOW ON AIR

Listen in Live

RIP! Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya Charles Njonjo ameaga dunia

Njonjo ambaye alitambulika kama 'The Duke of Kabeteshire' amefariki akiwa na umri wa miaka 101.

image
na Radio Jambo

Habari02 January 2022 - 07:28

Muhtasari


•Njonjo ambaye alitambulika kama 'The Duke of Kabeteshire' amefariki akiwa na umri wa miaka 101.

Marehemu Charles Njonjo alipokuwa anaadhimisha kuhitimu miaka 101

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa kwanza baada ya Kenya  kupata  uhuru, Charles  Mugane Njonjo amefariki dunia.

Waziri huyo wa zamani  wa Sheria na masuala  ya Katiba aliaga mwendo wa saa kumi na moja akiwa nyumbani kwake Muthaiga, Nairobi.

Njonjo ambaye alitambulika sana kama 'The Duke of Kabeteshire' amefariki akiwa na umri wa miaka 101.

Alipokuwa anathibitisha hayo, rais Uhuru Kenyatta amesema kifo cha Njonjo ni pigo kubwa kwa familia, marafiki, Kenya na Afrika yote kwa jumla.

Rais amemsherehekea marehemu kwa jukumu kubwa alilocheza katika ujenzi wa taifa  na kwa kazi nzuri aliyofanya kwa kujitolea alipofanywa mwanasheria mkuu wa kwanza baada ya nchi kupata uhuru.

"Kenya inafaa kumshukuru Mhe. Njonjo kwa utawala unaoendelea wa kikatiba na kisheria kwa kazi  yake nzuri alipohudumu kama Mwanasheria Mkuu wa kwanza wa nchi baada ya uhuru kati ya 1963 na 1979, na kama Waziri wa Masuala ya Katiba kati ya 1980 na 1983. Kwa niaba ya taifa la Kenya, familia yangu na kwa niaba yangu binafsi, natuma salamu za rambirambi kwa familia, marafiki na jamaa wa Mhe. Njonjo, na Wakenya wote." Rais amesema.

Rais ametakia familia ya Njonjo na Wakenya wote kwa jumla  neema na ujasiri wa kupambana na majonzi ya kupoteza shujaa huyo wa taifa.

"Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Mhe. Charles Mugane Njonjo kwa amani ya milele." Amesema rais Kenyatta.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved