logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Isaac Juma akamatwa

Kulingana na ripoti kutoka DCI, Juma alipatana na kifo hicho cha ghafla baada ya kumaliza kula chajio

image
na Radio Jambo

Yanayojiri27 January 2022 - 14:00

Muhtasari


  • Mtuhumiwa wa mauaji ya shabiki mahiri wa spoti Isaac Juma, 58, amekamatwa.
  •  Mtuhumiwa huyo kwa kwa jina Milton Namatsi, 27, amekamatwa nyumbani kwake Mumias na makachero wa kitengo cha DCI baada ya uchunguzi wa awali kuonesha kuwa Namatsi alikuwa na ushawishi mkubwa katika mauaji ya shabiki huyo wa spoti

Mtuhumiwa wa mauaji ya shabiki mahiri wa spoti Isaac Juma, 58, amekamatwa.

Mtuhumiwa huyo kwa kwa jina Milton Namatsi, 27, amekamatwa nyumbani kwake Mumias na makachero wa kitengo cha DCI baada ya uchunguzi wa awali kuonesha kuwa Namatsi alikuwa na ushawishi mkubwa katika mauaji ya shabiki huyo wa spoti.

Kulingana na ripoti kutoka DCI, Juma alipatana na kifo hicho cha ghafla baada ya kumaliza kula chajio na familia yake na alipotoka nje ya nyumba yake, inaripotiwa alikutana na watenda maovu hao wakiwa wanavizia katika ua la nyumba yake.

“Juma na familia yake walikuwa wamemaliza kupata chajio katika boma yake huko kijijini Ebuyenjeri, Mumias wakati wauaji hao walipovamia,"DCI Ilisema.

Watoto wao waliokuwa nje walihisi nyayo za watu una hapo wakaingia ndani kuripoti kwa wazazi ambao hawakuamini madai hayo ya Watoto ila muda mchache baadae walisikia zogo katika zizi la mbuzi na baadae kondoo kutoa milio nah apo ndipo marehemu Juma na kijana wake wa miaka 17 walipojitoma nje ili kuona kile kilichokuwa kikiwasibu kondoo wao.” Ilielezea Zaidi DCI

Kabla ya kufika kwenye zizi, watu waliokuwa wamejihami kwa mapanga walimdakia Juma mithili ya nyani adakiavyo ndizi na kumkatakata hadi kufa.

Kijana wake huyo alibahatika kuwapiga chenja wauaji hao na kukwepa kifo kwa tundu la sindano.

DCI pia imesema mauaji ya shabiki huyo wa spoti huenda yamesababishwa na mgogoro wa mashamba.

Marehemu ambaye anatajwa kuwa mchuuzi wa magazeti jijini Nakuru kabla ya kustaafu na kurudi nyumbani kwake Mumias alikuwa ni shabiki wa kufa kupona wa michezo nchini Kenya huku akitajwa kuwa mshupavu huyo namba moja wa timu ya taifa Harambee Stars na AFC Leopards.

Mtuhumiwa wa mauaji hayo amezuiliwa katika kituo cha polisi akisubiri kufikishwa mahakamani siku ya Ijumaa ya tarehe 28 Januari kwa kesi ya mauaji.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved