Raila Odinga aagizwa kufika mbele ya NCIC kufuatia matamshi yake "madoadoa"

Muhtasari

•NCIC inamtaka Raila aeleze matumizi yake ya hivi majuzi ya neno 'madoadoa' katika mkutano wa Azimio la Umoja wa hivi majuzi katika kaunti ya Wajir.

Image: TWITTER// RAILA ODINGA

Tume ya Tume ya Uwiano na Utangamano wa Kitaifa (NCIC) imeuagiza kinara wa ODM kufika mbele yake kufuatia matamshi "madoadoa" aliyotoa katika kaunti ya Wajir.

Kupitia taarifa iliyotolewa Ijumaa, NCIC imetaja matamshi hayo ambayo Raila alitoa Jumatano kuwa ya chuki.

"Tume ingependa kuwahakikishia Wakenya kuhusu kujitolea kwake kuzuia aina yoyote ya matamshi ya chuki ili kuhakikisha Kenya inasalia kuwa taifa tulivu, lenye ustawi na mshikamano na kutimiza ahadi yetu ya 'uchaguzi bila noma'," Taarifa ya NCIC ilisoma.

NCIC inamtaka Raila aeleze matumizi yake ya hivi majuzi ya neno 'madoadoa' katika mkutano wa Azimio la Umoja wa hivi majuzi katika kaunti ya Wajir.

Raila aliwaomba wakazi wa Wajir kuunga mkono wagombea wa vuguvugu la Azimio La Umoja katika uchaguzi mkuu wa mwezi Agosti.

Raila alisema kuwa vuguvugu hilo lina vyama vingi ambavyo vimeungana ili kuunganisha nchi, hivyo basi haja ya kulipigia kura.

Mengine yanafuata...