logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kenya yashindwa kulipa China deni la mkopo wa 18bn uliojenga Southern Bypass

Mkurugenzi wa hesabu za serikali anasema Kenya imeshindwa kulipa deni la mkopo wa 18bn kwa Uchina.

image
na Radio Jambo

Habari22 March 2022 - 09:20

Muhtasari


• Kulingana  na ripoti ya mkurugenzi mkuu wa hesabu za serikali, Nancy Gathungu, taifa la Kenya limekwama na kushindwa kulipa deni la mkopo wa bilioni 18 uliotumika kujenga barabara ya Southern Bypass. 

Rais Uhuru Kenyatta

Kenya ni miongoni mwa mataifa ya bara la Afrika ambayo yamewekeza sana katika miundo msingi ya kupendeza mno, ila kwa gharama ya mikopo haswa kutoka taifa la Uchina.

Kulingana na ripoti iliyochapishwa na gazeti moja la biashara nchini, Kenya imeshindwa kulipa deni la shilingi bilioni 18 ambazo ilikopa taasisi ya mikopo ya Uchina ili kufadhili ujenzi wa barabara ya Southern Bypass.

Kulingana na gazeti hilo, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Nancy Gathungu anasema Kenya sasa inadaiwa na Benki ya Exim ya China Shilingi bilioni 3.6 za malipo yaliyocheleweshwa kwa mwaka hadi Juni 2021. Hili ni ongezeko la Shilingi milioni 726 milioni kutoka Shilingi bilioni 2.9 ambazo zilikuwa bado hazijalipwa mwaka wa 2020.

Bi Gathungu sasa anaonya kwamba mlipa ushuru atalemewa na maslahi na adhabu zaidi ikiwa nchi haitadhibitisha ulipaji huo.

Ripoti hii ya ongezeko la mzigo wa madeni ya mikopo kwa wananchi linazidi kuongezeka huku pia kukiwa na taarifa zingine kwamba tayari nchi inatatizika kumudu gharama za juu za uendeshaji wa Reli ya kisasa (SGR) baada ya ukusanyaji wa mapato na kampuni ya Afristar kufuatilia matumizi na hivyo kuwasukuma walipa kodi kwa bili kubwa ya kuendeleza shughuli.

Kulingana na taarifa hiyo, Barabara ya Southern Bypass ilijengwa na Shirika la Barabara na Madaraja la China (CRBC) kwa kutumia mikopo kutoka Benki ya Exim ya China. Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara za Kenya (KeNHA) mnamo 2012 ilichagua CRBC kujenga barabara kuu ya njia nne za uchukuzi, kwa Shilingi bilioni 18 bilioni.

Barabara hiyo ambayo ilizinduliwa kwa matumizi na rais Uhuru Kenyatta pamoja na rais wa Tanzania hayati John Magufuli ina umbali wa kilomita 29.

 

- Gazeti la Business Daily


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved