KCSE 2021: Fahamu jinsi ya kujua matokeo yako

Muhtasari

•Magoha alitangaza matokeo ya mtihani huo katika makao makuu makuu ya KNEC adhuhuri ya Jumamosi.

Education CS George Magoha at KNEC headquarters during the release of the 2021 KCSE results on April,23,2022
Education CS George Magoha at KNEC headquarters during the release of the 2021 KCSE results on April,23,2022
Image: MERCY MUMO

Watahiniwa wa KCSE 2021 sasa wanaweza kujua jinsi walivyofanya baada ya waziri wa elimu George Magoha kutangaza matokeo ya mtihani huo.

Magoha alitangaza matokeo ya mtihani huo katika makao makuu makuu ya KNEC adhuhuri ya Jumamosi.

Watahiniwa wanaweza kujua matokeo yao kwa kutuma Index Number yao kwa nambari 20076. Mtahiniwa anaweza kutumia huduma yoyote ya simu kuangalia matokeo yake.

Takriban watahiniwa 826,015 walifanya mtihani wa KCSE 2021 katika vituo 10,413 kote nchini.

Haya ni matokeo ya mwisho ya waziri Magoha kutangaza katika utawala wa rais Uhuru Kenyatta.