KCSE 2021: Jariel Ndeda Obura ndiye bingwa kwa A ya pointi 87.167, Orodha ya wanafunzi 10 bora

Muhtasari

•Jariel Ndeda Obura kutoka shule ya upili ya Mang'u ndiye mwanafunzi bora katika KCPE 2021 baada ya kujizolea alama ya A ya pointi 87.167.

•Watahiniwa takriban 145, 000 waliweza kupata zaidi ya alama C+. Wote hao wataweza kujiunga na chuo kikuu kwa njia ya moja kwa moja.

Waziri wa Elimu George Magoha katika makao makuu ya KNEC wakati wa kutolewa kwa matokeo ya KCSE 2021 mnamo Aprili,23,2022.
Waziri wa Elimu George Magoha katika makao makuu ya KNEC wakati wa kutolewa kwa matokeo ya KCSE 2021 mnamo Aprili,23,2022.
Image: MERCY MUMO

Hatimaye matokeo ya mtihani wa KCSE 2021 yametangazwa.

Waziri wa elimu George Magoha alitangaza matokeo hayo katika makao makuu ya KNEC Jumamosi adhuhuri.

Jariel Ndeda Obura kutoka shule ya upili ya Mang'u ndiye mwanafunzi bora katika KCPE 2021 baada ya kujizolea alama ya A ya pointi 87.167.

Mukuha Timothy Kamau kutoka Alliance aliibuka wa pili na A ya pointi 87.139 . Alifuatwa na Job Ngala aliyepata 87.10 ambaye alikuwa mwanafunzi katika shule ya upili ya Mangu.

Wengine ni: 

4. Chege David Kamau- 87

5. Ramadhan Musa Tepo- 87.10

6. Mwendo Cicily Mutheu - 87.086

7. Ian Mwai Toyota - 87.08

8. Rita Shekina- 87.079

9. Mushindi Daniel Ouma- 87

10. Brenda Cherotich- 87

Antony Njuguna Muhoro kutoka shule ya msingi ya Kiamaina ndiye mwanafunzi bora kutoka shule ya kaunti ndogo.

Reuben Osolo kutoka shule ya upili ya Kapsabet ndiye mwanafunzi bora mwenye mahitaji maalum akizoa A ya pointi 84.

Katika mtihani wa KCPE 2020, mwanafunzi bora alikuwa Robinson Wanjala Simiyu kutoka Shule ya Upili ya Murang'a ambaye alipata A ya pointi 87.334. Wanjala alifuatwa na Allan Wasonga   kutoka Shule ya Upili ya Agoro Sare ambaye alijizolea pointi 87.173.

Takriban watahiniwa 826, 000 walifanya mtihani wa KCSE 2021 katika vituo 10,413 kote nchini.

Watahiniwa 1,138 walipata alama A. 789 kati yao ni wavulana huku wasichana waliopata A wakiwa 349. Wavulana 3819 waliweza kupata A- huku wasichana 2154 wakipata alama hiyo.

Watahiniwa takriban 145, 000 waliweza kupata zaidi ya alama C+. Wote hao wataweza kujiunga na chuo kikuu kwa njia ya moja kwa moja.

Visa 441 vya wizi wa mitihani vimeripotiwa katika KCSE 2021. Matokeo ya watahiniwa hao yamefutwa. Matokeo ya shule moja yamezuilia huku uchunguzi wa madai ya wizi ukiendelea.