Basi lililojaa abiria latumbukia kwenye mto Kisii

Ripoti zilidai kuwa abiria kadhaa walipata majeraha mabaya wakati wa ajali hiyo.

Muhtasari
  • Abiria waliojeruhiwa walipelekwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii, kilomita saba kutoka eneo la ajali
Image: KWA HISANI

Basi la abiria linalomilikiwa na kampuni ya huduma ya Guardian Bus limetumbukia kwenye mto Kisii.

Ripoti zilizofikia Radiojambo zinaonyesha kuwa mkasa huo ulitokea Nyamarambe kaunti ya Kisii.

Idadi kamili ya watu waliokuwa kwenye basi hilo haijajulikana.

Ripoti zilidai kuwa abiria kadhaa walipata majeraha mabaya wakati wa ajali hiyo.

Abiria waliojeruhiwa walipelekwa katika Hospitali ya Mafunzo na Rufaa ya Kisii, kilomita saba kutoka eneo la ajali.

Shughuli za uokoaji wa dharura zinaendelea kwa sasa, huku wakazi na watoa huduma wakiwasaidia majeruhi.

Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana hadi wakati wa kuchapishwa kwa habari hii.