Katibu wa kudumu wa Idara ya magereza, Esther Ngero ajiuzulu

Amehudumu kwa nafasi hiyo kwa miezi mitano tu.

Muhtasari

• Katika taarifa iliyochapishwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei siku ya Jumanne, Ngero alijiuzulu kwa sababu za kibinafsi.

• Taarifa hiyo ilifichua zaidi kwamba Ngero alijiunga na makatibu wakudumu Desemba 2022 baada ya kazi katika sekta ya mafuta kwa miongo miwili.

katibu wa kudumu wa Huduma za Urekebishaji, Esther Ngero
katibu wa kudumu wa Huduma za Urekebishaji, Esther Ngero

Katibu wa kudumu wa Huduma za magereza Esther Ngero amejiuzulu.

Haya yanajiri wiki moja baada ya kuhamishwa kutoka afis ya mkuu wa mawaziri akisimamia idara ya Utendaji na Usimamizi wa uwasilishaji hadi Idara ya Huduma za mahakama ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Utawala wa Kitaifa.

Katika taarifa iliyochapishwa na Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei siku ya Jumanne, Ngero alijiuzulu kwa sababu za kibinafsi.

“Mheshimiwa Rais amepokea na kukubali kwa masikitiko kujiuzulu kwa Esther Ngero, Katibu Mkuu wa Huduma za Urekebishaji, ambaye anaondoka madarakani kwa sababu zake binafsi,” ilisoma taarifa hio.

Koskei alibainisha kuwa Ngero amekuwa nguzo muhimu katika kuanzisha mfumo wa kitaasisi ili kusaidia utekelezaji wa Usimamizi na Ufuatiliaji wa Utendaji wa Utumishi wa Umma kwa Wizara, Idara za Serikali na mashirika ya serikali (MDAs).

Taarifa hiyo ilifichua zaidi kwamba Ngero alijiunga na makatibu wakudumu Desemba 2022 baada ya kazi katika sekta ya mafuta kwa miongo miwili.

Amehudumu kwa nafasi hiyo kwa miezi mitano tu.