Watu 6 wafariki baada ya kisima walikokuwa wakidensi juu kuporomoka na kuwameza

Watu 11 ambao walikuwa wamekwenda kuhudhuria hafla ya harusi Ruiru walikuwa wanacheza densi kwa mbwembwe juu ya kisima hicho kabla ya zege kuporomoka na kuingia ndani na waliokuwa juu yake.

Muhtasari

• Tukio hilo liitokea atika eneo la Kihunguro, Ruiru na walikuwa wanacheza densi kwa mbwembwe juu ya kisima kilichokuwa kimefunikwa kwa zege ya saruji

Crime Scene
Image: HISANI

Watu sita wameripotiwa kufariki dunia katika kaunti ya Kiambu baada ya kisima walichokuwa wamesimama juu yake kuporomoka.

Kwa mujibu wa ripoti ya Citizen, sita hao walikuwa wanatarajia kuhudhuria hafla ya harusi ya mmoja wa rafiki zao katika eneo la Kihunguro, Ruiru na walikuwa wanacheza densi kwa mbwembwe juu ya kisima kilichokuwa kimefunikwa kwa zege ya saruji.

Ghafla saruji hiyo iliporomoka na kuwameza sita hao kwenda ndani ya kisima hicho chenye kina cha urefu ambao hadi sasa haujabainika.

Citizen walisema Kulingana na polisi, takriban watu 11 walikuwa wakicheza kwenye zege ilipoanguka Jumamosi na wengine wakiokolewa, watu sita walikufa.

Mtoto mmoja alikuwa miongoni mwa waliokufa na Waliookolewa walipelekwa katika hospitali ya Ruiru.

Gavana wa Kiambu Kimani Wamatangi alithibitisha kisa hicho.

“Tangi la chini ya ardhi limeanguka Kihunguro karibu na Kituo cha Polisi cha Utawala katika Kaunti Ndogo ya Ruiru. Marafiki na familia walikuwa wakisherehekea harusi wakati tanki ilianguka na watu wapatao 30," The Star walimnukuu.

Taarifa hizi zinakuja siku chache tu baada ya watu wengine wawili kuripitiwa kufariki katika kaunti hiyo eneo la Thika Kiganjo baada ya kula ugali kutokana na unga waliookota kwenye eneo la kutupwa taka.

Taarifa za awali ziliripoti kwamba wawili hao walifariki hospitalini kutokana na makali ya kukeketwa kwa matumbo na wengine wasiopungua saba walikuwa wamelazwa hospitalini mmoja akiwa katika hali mbaya.

Simon Kioko, mmoja wa wale waliokula kipande cha Ugali waliotengeneza Jumatatu, aliambia runinga hiyo kuwa unga waliotumia ulitoka katika eneo kubwa la kutupa taka la Kiambu lililoko Kang'oki huko Thika.