logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Alfred Mutua,Kuria wahamishwa Ruto akifanya mabadiliko katika baraza la mawaziri

Waziri wa Maji Alice Wahome amebadilisha nyadhifa zake na Zachary Njeru wa Wizara ya Ardhi,

image
na Radio Jambo

Yanayojiri04 October 2023 - 17:57

Muhtasari


  • Moses Kuria amehamishwa kutoka hati yake ya Biashara hadi Wizara ya Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Uwasilishaji.

Rais William Ruto Jumatano usiku alipanga upya Baraza lake la Mawaziri, katika hatua iliyoshuhudia wizara mbalimbali zikiunganishwa na kubadilishwa jina.

Katika hatua hiyo, Rais Ruto alipanua Ofisi ya Waziri Mkuu na kujumuisha Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora, inayoongozwa na Musalia Mudavadi.

Moses Kuria amehamishwa kutoka hati yake ya Biashara hadi Wizara ya Utumishi wa Umma, Utendaji na Usimamizi wa Uwasilishaji.

Alfred Mutua, kwa upande mwingine, anaondoka katika wizara ya Mashauri ya Kigeni kuongoza wizara ya Utalii na Wanyamapori.

Waziri wa EALA Rebecca Miano kwa upande wake amehamishwa hadi kwenye wizara ya Biashara na Viwanda kuchukua nafasi ya aliyekuwa Mbunge wa Gatundu Kusini.

Waziri wa Maji Alice Wahome amebadilisha nyadhifa zake na Zachary Njeru wa Wizara ya Ardhi, Kazi za Umma na Maendeleo ya Miji.

 

 

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved