Wafanyakazi wawili wa kampuni ya Usalama watoweka na Sh94m za Quickmart

Gari hilo lilipatikana likiwa limetupwa katika eneo moja jijini Nairobi.

Muhtasari

• Pesa hizo zilitoka kwenye chumba cha kuhifadhia mali cha kampuni ya ulinzi katika eneo la Industrial Area na zilipaswa kuwasilishwa kwa benki iliyoko katikati mwa Jiji .

• Polisi walisema waliomsindikiza waligundua gari lililokuwa na pesa halikuwepo dakika chache baada ya kuondoka na pesa taslimu.

PESA ZA KENYA
PESA ZA KENYA
Image: STAR

Polisi Jumatatu walianzisha msako wa kuwatafuta wafanyikazi wawili wa kampuni ya ulinzi walioiba Sh94.9 milioni walizopaswa kuwasilisha katika benki moja jijini Nairobi.

Pesa hizo zilitoka kwenye chumba cha kuhifadhia mali cha kampuni ya ulinzi katika eneo la Industrial Area na zilipaswa kuwasilishwa kwa benki iliyoko katikati mwa Jiji .

Ilikuwa ya maduka makubwa ya Quickmart na ilikuwa ya mauzo ya wikendi, polisi walisema.

Wawili hao, waliokuwa kwenye gari la kampuni hiyo, walikuwa wamefika kwenye chumba hicho kama ilivyoratibiwa lakini waliondoka bila kusindikizwa na polisi.

Polisi walisema waliomsindikiza waligundua gari lililokuwa na pesa halikuwepo dakika chache baada ya kuondoka na pesa taslimu.

Gari hilo lilipatikana likiwa limetupwa katika eneo moja jijini Nairobi.

Maafisa wakuu wa polisi walitembelea eneo la tukio na kubaini kuwa wawili hao walitoroka na gari lililokuwa likiwasubiri.

Polisi waliotembelea eneo la tukio walidgibitisha  kuwa uchunguzi umeanzishwa wa kuwanasa washukiwa hao.

Vikundi vya maafisa wa usalama viliamrishwa kuwafuata wawili hao lakini wakaripoti kuwa walikuwa wametorokea kusikojulikana.

Polisi wanasema tukio hilo ni jipya kwa sasa na linaonekana kuwa kazi ya ndani.

Maafisa ambao walipaswa kusindikiza gari lililohusika katika wizi huo walihojiwa kama sehemu ya uchunguzi wa tukio hilo.