Henry Rotich yuko huru katika kesi ya bwawa la Arror na Kimwarer

Wakati wa uamuzi huo, ilibainika kuwa waziri huyo wa zamani hakuwa na kesi ya kujibu

Muhtasari
  • Wakati wa uamuzi huo, ilibainika kuwa waziri huyo wa zamani hakuwa na kesi ya kujibu licha ya mlipa ushuru kupoteza Ksh63 bilioni.

Aliyekuwa Waziri wa Hazina Henry Rotich aliachiliwa huru  Alhamisi na mahakama  katika kesi ya  Kashfa ya Arror na Kimwarer.

Wakati wa uamuzi huo, ilibainika kuwa waziri huyo wa zamani hakuwa na kesi ya kujibu licha ya mlipa ushuru kupoteza Ksh63 bilioni.

Mahakama imesema kuwa hakuna ushahidi wa kutosha dhidi ya waziri huyo wa zamani.

“Washtakiwa wote katika kesi hii wanaachiwa huru chini ya kifungu cha 210 kutokana na kukosekana kwa ushahidi kutokana na upande wa mashtaka kupuuza wajibu wake,” ilisomeka sehemu ya uamuzi huo

Rotich alituhumiwa kufuja pesa za ujenzi wa mabwawa hayo.

Mengi yafuata;