Linturi aondolewa mashtaka yote kuhusiana na uuzaji mbolea feki

Kamati hiyo iliyosimamiwa na Mwakilishi wa Kike wa Marsabit, Bi Naomi Waqo, ilipuuzilia mbali mashtaka yaliyowasilishwa na mbunge wa Bumula,

Muhtasari
  • Wabunge saba kati ya 11 kwenye kamati hiyo, walipiga kura ya kumwokoa Bw Linturi, wakisema kwamba mbunge huyo wa zamani wa Igembe Kusini hakuhusika moja kwa moja katika kashfa hiyo.
Waziri wa Kilimo Mithika Linturi mnamo Aprili 8, 2024. Picha: EZEKIEL AMING'A
Waziri wa Kilimo Mithika Linturi mnamo Aprili 8, 2024. Picha: EZEKIEL AMING'A

Waziri wa Kilimo Mithika Linturi ameondolewa mashtaka yote kuhusiana na uuzaji wa mchanga ukisemekana kuwa mbolea, huku wabunge wa Upinzani wakilaumu wenzao wa upande wa Serikali katika kamati iliyoteuliwa na bunge.

Wabunge saba kati ya 11 kwenye kamati hiyo, walipiga kura ya kumwokoa Bw Linturi, wakisema kwamba mbunge huyo wa zamani wa Igembe Kusini hakuhusika moja kwa moja katika kashfa hiyo.

Kamati hiyo iliyosimamiwa na Mwakilishi wa Kike wa Marsabit, Bi Naomi Waqo, ilipuuzilia mbali mashtaka yaliyowasilishwa na mbunge wa Bumula, Bw Jack Wanami Wamboka kuhusu sakata ya usambazaji wa mbolea feki.

Hoja yake ilipitishwa na wabunge 149 kati ya 188 waliokuwa bungeni wiki mbili zilizopita. Wabunge 36 waliipinga lakini kamati ikaundwa kufuatilia na kuchunguza madai hayo.

Wabunge saba kati ya 11 walipiga kura kuokoa CS.

Mbunge Wamboka alikuwa ameorodhesha sababu tatu katika hoja ya kumtimua CS Linturi: ukiukaji mkubwa wa Katiba au sheria nyingine yoyote, sababu kuu za kuamini kuwa Waziri huyo ametenda uhalifu chini ya sheria za kitaifa, pamoja na utovu wa nidhamu mkubwa.

Madai hayo yanahusu ununuzi na usambazaji wa mbolea ya ruzuku ya serikali ambayo yenyewe iko chini ya uchunguzi juu ya wasiwasi kuwa ilikuwa bandia.