Wikendi ndefu! Serikali yatangaza Jumatatu, Juni 17 kuwa Sikukuu ya Umma

Sikukuu hiyo imetangazwa kuadhimisha Eid-Al-Adha.

Muhtasari

•Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki ametangaza Jumatatu, Juni 17 kuwa sikukuu ya umma.

Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI KITHURE KINDIKI Waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki
Image: KWA HISANI

Jiandae kwa wikendi ndefu!

Serikali ya Kenya, kupitia waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki imetangaza  siku ya Jumatatu, Juni 17 kuwa sikukuu ya umma.

Sikukuu hiyo imetangazwa kwenye gazeti rasmi ya serikali. Siku hiyo imetengwa kuadhimisha Eid-Al-Adha.

Sherehe ya Eid-ul-Adha ni kukumbuka kujitolea kwa Nabii Ibrahim kwa Mwenyezi Mungu na utayari wake wa kumchinja mwanawe, Ismail.

Sikukuu ya Sadaka ni mojawapo ya sikukuu mbili muhimu za Uislamu.

Ni muhimu hasa kwa sababu ni alama ya mwisho wa Hija ya kila mwaka au Hija ya Makka, inayoadhimishwa katika mwezi wa mwisho wa kalenda ya Kiislamu.