logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Seneta wa Marsabit Mohammed Chute akamatwa

Seneta huyo anahusishwa na ufisadi wa mamilioni katika serikali ya kaunti ya Marsabit.

image

Habari11 July 2024 - 12:57

Muhtasari


  • Msemaji wa EACC Eric Ngumbi amethibitisha kuwa Chute anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Integrity Center.

Seneta wa Marsabit Mohammed Chute amekamatwa na maafisa kutoka Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC).

Msemaji wa EACC Eric Ngumbi amethibitisha kuwa Chute anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Integrity Center.

Seneta huyo anatuhumiwa kwa mgongano wa kimaslahi na anahusishwa na ufisadi wa mamilioni katika serikali ya kaunti ya Marsabit.

Kufuatia kukamatwa kwake, tume ya kukabiliana na ufisadi iliapa kuchunguza madai yaliyotolewa dhidi ya seneta huyo na kwamba maelezo zaidi yatatolewa kwa wakati ufaao.

Kukamatwa kwa Chute kunajiri siku moja tu baada ya kuandamana na Rais William Ruto wakati wa uzinduzi wa Kituo Kidogo cha Kimuka, Kajiado.

Wakati wa mkutano wake na Mkuu wa Nchi, Chute alimpongeza Rais kwa kutenga Ksh1 bilioni kwa ajili ya ufugaji wa mifugo kwa wafugaji katika kaunti ya Marsabit.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved