Watu kadhaa wahofiwa kufariki katika ajali mbaya Kericho

Polisi walisema ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa trela kutoka Kipsitet General aliposhindwa kulidhibiti.

Muhtasari

•Polisi wamethibitisha kuwa mwanamume mmoja amefariki katika ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa saba unusu mchana.

Dereva wa trela kisha aliondoka kwenye njia yake na kugonga matatu ya Toyota, ambapo mwanamume mmoja alifariki papo hapo.
Dereva wa trela kisha aliondoka kwenye njia yake na kugonga matatu ya Toyota, ambapo mwanamume mmoja alifariki papo hapo.
Image: HISANI

Watu kadhaa wanahofiwa kufariki katika ajali ya barabarani iliyohusisha gari la PSV na trela katika kaunti ya Kericho.

Polisi wamethibitisha kuwa mwanamume mmoja amefariki katika ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa saba unusu mchana.

Polisi walisema ajali hiyo ilitokea wakati dereva wa trela kutoka Kipsitet General aliposhindwa kulidhibiti eneo la Kisumu Ndogo.

Dereva wa trela kisha aliacha njia yake na kugonga matatu ya Toyota, ambapo mtu mmoja alikufa papo hapo.

"Kutokana na athari hiyo abiria kadhaa wanahofiwa kufariki, taarifa zaidi zitafuata punde tu tutakapoondoa matatu ili kuthibitisha ikiwa tuna miili iliyonasa," polisi walisema.