Wanafunzi 17 wateketea hadi kufa katika shule moja ya msingi Nyeri

Moja ya mabweni ya shule hiyo liliteketea na kuwaua wanafunzi 16.

Muhtasari

•Msemaji wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi Resila Onyango ameithibitishia Radio Jambo kisa hicho.

•Wanafunzi wengine 14 wanaendelea kupokea matibabu baada ya kupata majeraha katika tukio hilo la kuhuzunisha.

Picha ya nyumba inayowaka moto
Image: MAKTABA

Takriban wanafunzi 17 wamethibitishwa kufariki katika shule ya Hillside Endarasha Academy katika eneo la Kieni, Nyeri, kufuatia mkasa wa moto Alhamisi usiku.

Idadi hii imeongezeka baada ya mwanafunzi mmoja zaidi kufariki. Msemaji wa  idara ya polisi Resila Onyango ameithibitishia Radio Jambo kisa hicho.

Moja ya mabweni ya shule hiyo liliteketea na kuwaua wanafunzi hao na kujeruhi wengine wengi.

Wanafunzi wengine 14 wanaendelea kupokea matibabu baada ya kupata majeraha katika tukio hilo la kuhuzunisha.

Naibu Mkurugenzi wa DCI John Onyango, Msaidizi Mwandamizi IG na Mkurugenzi Kitengo cha Mauaji na Kitengo cha Kudhibiti Maafa cha NPS wako njiani kuelekea eneo la tukio.