Mahakama yamzuia gavana Mutua kugura Azimio

Muhtasari

•Mahakama imetupilia mbali malalamiko ya MCC kwa misingi kwamba yaliwasilishwa kabla ya wakati wake.

•Mlalamishi Martin Mugo Maina alidai msajili wa vyama vya siasa alikiorodhesha chama cha Maendeleo Chap Chap bila kufuata taratibu.

Kiongozi wa chama cha Maendeleo Chap Chap Alfred Mutua atia saini makubaliano na Naibu Rais William Ruto, huku Moses Wetangula na Musalia Mudavadi wakiwapo. Aliiondoa Azimio la Umoja kwa Kenya Kwanza mnamo Jumatatu, Mei 9
Kiongozi wa chama cha Maendeleo Chap Chap Alfred Mutua atia saini makubaliano na Naibu Rais William Ruto, huku Moses Wetangula na Musalia Mudavadi wakiwapo. Aliiondoa Azimio la Umoja kwa Kenya Kwanza mnamo Jumatatu, Mei 9
Image: DPPS

Mahakama ya mizozo ya vyama imekisimamisha chama cha Maendeleo Chap Chap kinachoongozwa na Gavana Alfred Mutua , Maendeleo Chap Chap (MCC) kujiondoa katika muungano wa Azimio la Umoja One Kenya.

Katika kikao cha Jumanne mahakama ilitupilia mbali malalamiko ya MCC kwa misingi kwamba yaliwasilishwa kabla ya wakati wake.

Pia imeamua kuwa MCC inapaswa kwanza kutumia mbinu za utatuzi wa migogoro ya ndani kabla ya kupeleka malalamishi mahakamani.

Chama cha MCC kiliwasilisha kesi mahakamani siku ya Jumatatu kikisema kuwa hakifahamu yaliyomo kwenye mkataba wake na muungano na Azimio la Umoja.

Waliomba maagizo ya kusimamisha notisi ya gazeti la serikali ya Aprili 14, 2022, ambayo iliorodhesha chama hicho kama mwanachama wa  muungano cha Azimio la Umoja-One Kenya.

Mlalamishi Martin Mugo Maina alidai msajili wa vyama vya siasa alikiorodhesha chama cha Maendeleo Chap Chap bila kufuata taratibu.

"Mshtakiwa wa pili alimuorodhesha mlalamishi kuwa ni mwanachama wa mshtakiwa wa Kwanza kupitia notisi ya gazeti la serikali ya tarehe 14 Aprili 2022 bila ya kuthibitishwa kwa azimio hilo na bila kufuata utaratibu wa katiba ya chama" Sehemu ya ombi lililowasishwa mahakani ilisoma.

Mlalamishi huyo aliendelea kusema kuwa chama cha Maendeleo Chap Chap kilijumuishwa katika muunganowa Azimio bila kufuata taratibu za Katiba ya Chama na bila ya kibali cha chombo husika cha chama na hivyo muungano huo ni batili.

(Utafsiri: Samuel Maina)