Fahamu 'Bifu' za Diamond na wasanii wenzake

Diamond ni msanii ambaye amevutia upendo na chuki kutoka kwa watu wengi.

Muhtasari

• Licha ya kuenziwa na wasanii wengi Diamond pia amekashifiwa sana na baadhi ya wasanii ambao amefanya nao kazi wakimshtumu kwa kuwadhulumu. 

Image: HILLARY BET

Bila shaka, bosi wa WCB Naseeb Abdul Juma almaarufu  Diamond Platnumz ni miongoni mwa wasanii tajika barani Afrika na kote duniani.

Diamond ni msanii mmoja ambaye ameweza kuvutia upendo na chuki kutoka kwa mashabiki wengi wa muziki pamoja na wasanii wenzake.

Katika grafiki hii tunaangazia baadhi tu ya wasanii mashuhuri ambao staa huyo wa Bongo anadaiwa kuwahi kuzozana nao.