Fahamu kaunti ambazo wanaume wana wapenzi wengi zaidi

Kaunti za Narok, Elgeyo Marakwet na Pokot Magharibi zinaongoza katika orodha hiyo.

Muhtasari

•Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya iliachia ripoti kuhusu Utafiti wa idadi ya watu na afya mwaka wa 2022.

Kaunti ambazo wanaume wana wapenzi wengi zaidi
Image: WILLIAM WANYOIKE

Siku ya Jumanne Januari 17, Ofisi ya Kitaifa ya Takwimu ya Kenya iliachia ripoti kuhusu Utafiti wa idadi ya watu na afya mwaka wa 2022.

Utafiti huo ulifanyika kati ya Februari 17 hadi Julai 13 kati ya wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 na wanaume miaka 15 hadi 54.