Wachezaji waliofungia vilabu vyao mabao mengi EPL

Salah alivunja rekodi ya Liverpool alipoifunga Man U mabao mawili.

Muhtasari

•Salah alifunga bao lake la 128 na 129 katika mechi 205 za ligi akiwa na Liverpool na kuwa mfungaji mabao bora wa muda wote wa klabu hiyo.

Wachezaji waliofungia vilabu vyao mabao mengi EPL
Image: WILLIAM WANYOIKE

Jumapili iliyopita, mshambulizi matata Mohammed Salah alifunga bao lake la 128 na 129 katika mechi 205 za ligi akiwa na Liverpool na kuwa mfungaji mabao bora wa muda wote wa klabu hiyo.

Mabao yake mawili dhidi ya Manchester United yalimsaidia kuvunja rekodi ya Robbie Fowler kama mfungaji bora wa Liverpool katika historia ya Ligi Kuu.

Hapa tumeorodhesha wachezaji wengine ambao walifungia vilabu vyao mabao mengi zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza.

  • Tottenham: Harry Kane – Mabao 201 (2009- hadi sasa)
  • Man City: Sergio Aguero –Mabao 184 (2011-2021)
  • Man United: Wayne Rooney- Mabao 183 (2002-2017)
  • Arsenal: Thiery Henry- Mabao 175 (1999-2012)
  • Newcastle: Allan Shearer- Mabao 148 (1996- 2006)
  • Chelsea: Frank Lampard- Mabao 147 (2001-2014)
  • Liverpool: Mohammed Salah – Mabao129 (2017-hadi sasa)
  • Everton: Romelu Lukaku – Mabao 68 (2013-2017)
  • Crystal Palace: Wilfred Zaha- Mabao 67 (2014- hadi sasa)
  • Westham United: Antonio- Mabao 59 (2015- hadi sasa)