logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Wafahamu wanasoka chipukizi wa Kenya waliojiunga na akademi za EPL

Mwaka wa 2021, mwanasoka mchanga wa Kenya, Leo Messo alijunga na akademi ya Arsenal akiwa na umri wa miaka 10.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri19 April 2023 - 10:22

Muhtasari


•Hivi majuzi, Aymen Onyango, alijiunga na timu ya Manchester City ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 9.

•Mwaka wa 2021, mwanasoka mchanga wa Kenya, Leo Messo alijunga na akademi ya Arsenal akiwa na umri wa miaka 10.

Hivi majuzi, mtoto wa meneja wa maendeleo katika Ligi ya Raga ya Kenya, Lucas Onyango, Aymen Onyango, alijiunga na timu ya Manchester City ya wachezaji wa chini ya umri wa miaka 9.

Onyango alizamia kwenye mtandao wa Twitter siku ya Jumatatu jioni kufichua habari hizo:

Mtoto wetu Aymen Onyango sasa ni mchezaji rasmi wa Manchester City baada ya kusajiliwa kwa vijana wa chini ya miaka 9. Katika maisha yangu sijawahi kujivunia hivi na kijana huyu amefanya bidii kufika hapa, safari inaanza sasa hivi anaendelea na akademi. . Sote tumefurahi," Onyango alitweet.

Aymen sio mchezaji chipukizi wa kwanza kutoka Kenya kuwahi kujiunga na akademi za vilabu bora vya EPL.

Mwaka wa 2021, mwanasoka mchanga wa Kenya, Leo Messo alijunga na akademi ya Arsenal akiwa na umri wa miaka 10.

Tyler Onyango amekuwa katika klabu ya Everton tangu mwaka wa 2011 ambapo alijiunga na akademi yao akiwa na miaka 8.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved