Nguli wa muziki wa reggae na dancehall kutoka Jamaica, Richell Bonner almaarufu Richie Spice ameratibiwa kutumbuiza moja kwa moja katika uwanja wa KICC, jijini Nairobi mnamo Mei 27 mwaka huu.
Mwimbaji huyo wa kibao 'Gideon Boots' pia anatarajiwa kuwatumbuiza mashabiki wake mjini Kisumu mnamo Mei 28.
Ziara ijayo ya Richie Spice haitakuwa yake ya kwanza nchini Kenya kwani aliwahi kutumbuiza tena humu nchini mwaka wa 2017 na 2019. Waimbaji wengine mahiri kutoka Jamaica wakiwemo Tarrus Riley, Glen Washington, Konshens, Cecile, Chris Martins na wengineo pia wametumbuiza Kenya miaka ya hivi majuzi.
Konshens alikuwa msanii wa Jamaica wa hivi majuzi kutumbuiza Kenya.